Na Joseph Ngilisho ARUSHA,
WAHITIMU wa Mafunzo katika Sekta ya Afya wametakiwa kuzingatia weredi katika taaluma yao na kujiepusha na vitendo viovu vya kuomba na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa , kutunza Siri za taasisi wanazofanyia kazi na kuacha kushinda wakichati na simu na kusahau majukumu yao .
Kauli hiyo imetolewa Jana na kaimu mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha, dkt Charles Migunga wakati alipohudhulia Mahafali ya 35 ya chuo Cha afya CEDHA cha jijini Arusha ,ambapo wanachuo wapatao 45 wanahitimu mafunzo ya miaka mitatu ya sekta ya Afya ngazi ya cheti na Diploma.
Alisema kuwa wizara ya Afya ipo kwenye malengo Muhimu ya kuboresha huduma ya Afya na watumishi wake,hivyo watumishi wa Afya wanapaswa kuzingatia maadili waliofundishwa na kujitenga na matendo maovu kwani serikali haitawafumbia macho na suala la mmomonyoko wa maadili kimekuwa likitajwa sana katika sekta ya Afya.
Alisema wizara ya Afya imeanza kutekelezwa Mpango huo wa maendeleo ya Afya ya Msingi(MMAM),na mojawapo ya malengo mahsusi ni kuhakikisha kuwa huduma za Afya zinakuwa karibu na wananchi .
Alisema mkakati huo unahitaji kujenga vituo vipya vya huduma ya Afya na kuandaa watumishi wengi wa Afya ambao wataendesha huduma hizo Katika ngazi mbalimbali za huduma za Afya hususani kwenye ngazi ya jamii ,zahanati na vituo vya afya.
"Hivyo ninyi wahitimu mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa mpango huu unatekelezwa kwa ufanisi Katika sehemu zenu za kazi kwa kutumia Maarifa na Ujuzi mlioupata Katika mafunzo yenu"alisema
Aidha alikipongeza chuo Cha CEDHA kwa jukumu la kuisaidia serikali kutekeleza mpango wa MMAM kwa kuandaa wakufunzi wa watumishi wa Afya na kutoa rai kwa chuo hicho kuendeleza kutoa mafunzo yenye ubora wa hali ya juu na kutoa wahitimu wengi zaidi
Awali kaimu Mkuu wa chuo hicho ,dkt Johannes Lukumay alisema kuwa wahitimu wa mafunzo hayo ya miaka mitatu wapo 45 ambao ni wa ngazi ya ualimu wa watumishi wa Afya wapatao 4,mafunzo ya Sayansi ya Taarifa za afya 38 na wahitimu wa uendeshaji na usimamizi wa huduma za Afya ni watatu.
Aidha aliongeza kuwa lengo la chuo Cha CEDHA ni kuimarisha na kusaidi mfumo wa huduma za afya kupitia maendeleo ya rasilimali watu chini ya programu mbalimbali za elimu,katika kozi ndefu na fupi ikiwemo mafunzo kwa watoa huduma za afya ,elimu ya watumishi wa afya ,ngazi ya cheti na diploma.
Ends...
0 Comments