TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA WAZALISHAJI WA ALMASI AFRIKA

 


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 


WAZIRI wa Madini nchini,dkt.Dotto Biteko amesema kwamba licha ya changamoto ya janga la UVIKO-19 Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mauzo ya madini aina ya almasi katika soko la dunia.

Waziri Biteko ametoa kauli hiyo leo wakati akitambulisha mkutano wa tatu wa baraza la mawaziri wa jumuiya ya nchi za Afrika zinazozalisha almasi(ADPA) unaotarajia kufanyika kesho  (leo)jijini Arusha ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo.


Akizungumza katika mkutano huo waziri Biteko alisema kwamba baada ya janga la UVIKO-19 bei ya almasi duniani ilianguka na  lakini kwa sasa almasi imepanda juu na kuifanya Tanzania kuendelea kufanya vizuri duniani.

"Katika kipindi cha janga la UVIKO-19 bei ya almasi ilianguka kwa kiasi kikubwa duniani na bei iliyokuwa juu ni dhahabu ila kwa sasa bei ya Almasi imepanda na kurudi katika hali yake ya kawaida  na uzalishaji wa juu kabisa wa Almasi hapa nchini ulikuwa ni mwaka 1977 ambapo kareti 300,077 zilizalishwa na mwaka wa fedha 1920 kareti 500,000 zilizalishwa ikiwa ni kiwango cha juu kabisa"alisema

Waziri Biteko alisema kuwa hivi karibuni kupitia mgodi wa almasi wa Mwadui uliopo mkoani Shinyanga serikal imeuza jiwe moja la almasi lenye kareti sita kwa thamani ya dola milioni 12 katika soko la dunia jambo ambalo linaashiria mafanikio makubwa kwa nchi.

“Huu uzalishaji haujawahi kutokea katika mgodi wetu wa Mwadui kwani tumeuza jiwe moja la almasi ya pink kwa thamani ya dola milioni kumi na mbili haya ni mafanikio makubwa sana kwa nchi yetu “alisema Biteko 

Waziri Biteko alisema kwamba pamoja na mgodi wa Mwadui kusimamisha uzalishaji kwa muda kutokana na ukarabati lakini kwa sasa serikali imeongeza hisa kutoka asilimia 25 mpaka 35 kama juhudi za kuongeza uzalishaji wa almasi duniani.

Akizungumzia mkutano wa baraza la mawaziri kwa nchi zinazozalisha almasi barani Afrika waziri Biteko alisema kwamba lengo la mkutano huo ni kuidhinisha nyaraka muhimu za baraza hilo,kuteua sekretarieti sanjari na kuhakikisha nchi za Afrika zinakuwa na sauti moja katika kusimamia rasiliamali hiyo.



Waziri Biteko alisisitiza kuwa wajumbe wa baraza hilo wataupitia upya mfumo wa umoja huo na kujifunza katika eneo la usimamizi wa madini ya almasi barani Afrika.

Alisema kuwa duniani kote madini ya almasi yana urasimu na mlolongo mpana hivyo mkutano huo itawapa fursa wajumbe kusimama na kuangalia vigezo kwa baadhi ya nchi barani Afrika zilizopigwa marufuku kufanya biashara ya almasi duniani.

“Tutaupitia upya mfumo wa umoja wetu ikiwemo katiba na kuboresha miongozo mbalimbali katika eneo la usimamizi wa madini ya almasi Bara Afrika “alisisitiza Biteko 

Tanzania ni mwenyekiti na mwenyeji wa mkutano wa ADPA ambapo umoja huo unajumuisha nchi 18 barani Afrika ambapo nchi 12 wanachama na 6 ni waangalizi. 

Ends...

Post a Comment

0 Comments