Na Joseph Ngilisho Arusha
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye leo Ijumaa Julai 22, 2022 amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Rais Ndayishimiye amechukua nafasi ya Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti huyo ametangazwa leo na Rais Kenyatta katika kikao cha kawaida cha 22 cha Wakuu wa nchi za Afrika ya Mashariki kilichofanyika leo jijini Arusha.
0 Comments