KIKONGWE ACHAFUKWA,AVUNJA NYUMBA ZAKE ZA MAMILIONI KUKWEPA KERO ZA WATOTO"Mkajenge zakwenu"

 


Na Joseph Ngilisho, ARUSHA 

Mzee mwenye umri wa miaka 89,Iddy Nzella Maganga ameamua kuzivunja nyumba  zake 2,zenye thamani ya sh,mil 200,zilizopo Ngarenaro NHC, jijini Arusha ,kwa madai kwamba baadhi ya watoto wake wanataka kumdhulumu akimtuhumu mmoja wapo kumfungia kwenye chumba cha giza kwa wiki moja, bila kumpatia chakula wala mahitaji muhimu .

Akiongea na waandishi wa habari huku akilia kwa uchungu,Maganga ambaye alifiwa na mke wake wa ndoa , alisema kuwa uamuzi wa kuzivunja nyumba hizo ni baada ya kubaini kwamba baadhi ya watoto wake wakiongozwa na Abdalah Maganga  wanania ovu juu ya mali zake na huenda akafa siku sio nyingi .




Alisema kuwa uamuzi huo ameuchukua akiwa na akili timamu na amefanya hivyo ili kuwakomesha watoto wasiotaka kufanyakazi wakisubiri mali za urithi .

"Hii nyumba ni mali yangu nilijenga na mke wangu ambaye kwa sasa ni marehemu,huyu mtoto Abdalah alinifungia ndani wiki moja nikiwa nakula kinyesi changu sijitambuli na nilikuja kuokolewa na mtoto wangu wa kike aitwaye Jasimin na mme wake baada ya kuvunja kitasa na kunitoa na kunipeleka hospitali "

"Jirani yangu anaitwa mama Masawe ambaye nilikuwa nikienda kuchukua chakula kwake alimpigia simu mtoto wangu Jasimini na kumwambia kuwà mbona mzee Abdalah  haonekani siku ya nne akija kuchukua chakula ,ndipo Jasimini na mumewe walipokuja na kukuta Abdalah amenifungia ndani " alisema 




Mzee huyo  ambaye anawatoto sita, kwa sasa anaishi kwa mtoto wake eneo la Kwa Morombo ,akidai kwamba Abdala alikuwa na nia mbaya juu yake, kutaka afariki dunia ili ajimilikishe nyumba hiyo kinyume cha sheria.

Alisema licha ya kuwa hiyo nyumba ni mali yake lakini Abdala alikuwa hamruhusu baba yake kuingia ndani  ya nyumba hiyo na pale anapokuwa akija kutafuta msaada kwa kijana huyo, alikuwa akifunga milango na geti la kuingilia .

Mzee Maganga alisisitiza kwa kutaka Abdala na Mwenzake Ridhiki Maganga kukaa mbali na mali zake watafute mali zao kwani baada ya kufanikiwa kubomoa nyumba hiyo anampamgo wa kuliuza eneo hilo muda wowote kuanzia sasa.

"Baada ya kupata fahamu nilianza taratibu za kuuza nyumba  yangu lakini kila nikifika na mteja hafungiwa nje na mwanangu Abdalah  hataki niingie ndani hata kujisaidia"alisema



Naye mtoto Jasimin Maganga alisema kuwa alimwokoa baba yake akiwa kwenye hali mbaya baada ya kumkuta hajitambui amefungiwa kwenye chumba kidogo kwa wiki moja bila kupatiwa chakula wala maji.

"Nilimkuta baba yangu akiwa kwenye hali mbaya sana alikuwa haongei chumba kilikuwa na giza kimefungwa na kinanuka kinyesi na alikuwa akila kinyesi chake ,nilimpeleka hospitali na baada ya kupatiwa matibabu alipata nafuu na kurejea katika hali ya kawaida na sasa naishi naye"alisema.

Kwa upande wake Abdalah  Maganga alikanusha taarifa za baba yake kumfungia kwenye chumba kwa wiki nzima bila chakula ,akidai kwamba taarifa hizo hazina ukweli .




Abdalah alikiri kuwa nyumba hiyo ni mali ya baba yake na marehemu mama yake ila yeye alikuwa akiishi hapo kama mwangalizi,na ameshtushwa sana kuona kundi la watu zaidi ya 50 kuvamia nyumba hiyo siku ya jumamosi wiki iliyopita na kufanya uharibifu.

Alisema mara baada ya kundi hilo kuvamia alijitahidi kutafuta msaada polisi lakini hakupata msaada wowote kwa wakati na polisi walifika kwa kuchelewa na  kukuta tayari nyumba zote zimevunja na vitu kutolewa nje.

"Mimi sina ugomvi na baba yangu ila sina mawasiliano naye kwa muda baada ya kuchukuliwa na kuishi na mdogo wangu Jasimini ,nitakachofanya kwa sasa ni kumwachia mungu tu"alisema Abdalah. 

Hata hivyo mdogo wake na  Mzee Maganga,Hasan Abdalah  alisema hana mawasiliano na kaka yake na kushauri kuwa kitendo kilichotokea kinapaswa kumalizika kisheria mahakamani.

Ends... 










Post a Comment

0 Comments