BY NGILISHO TV
Siku moja baada ya kuapishwa kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camilius Wambura ametoa rai kwa wananchi kutoa taarifa iwapo wataona tukio la kihalifu huku akionya wanaojihusisha na vitendo hivyo watachukuliwa hatua.
Akiwa mkoani Arusha kwenye mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Wambura amesema ni jukumu la jeshi hilo kulinda viongozi na wananchi.
Hili ni jukumu la kwanza la Wambura akionekana hadharani tangu ateuliwe juzi Jumanne na kuapishwa jana Jumatano Julai 20, 2022 baada ya kuhudumu katika nafasi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kwa takriban mwaka mmoja.
0 Comments