Na Joseph Ngilisho, Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha ,Said Mtanda amesitisha tenda mpya ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu iliyokuwa ianze agost mosi mwaka huu na kuwataka wakandarasi wenye mikataba ya zamani kuendelea na kazi hiyo hadi pale tenda mpya itakapotangazwa rasmi .
Aidha amewaonya wakandarasi wa taka ambao waliacha kukusanya taka kwa kisingizio cha tenda mpya kuwa atawachukulia hatua kali za kisheria kwa kusababisha jiji kuwa chafu.
"Naagiza wakandarasi wote wanaozoa taka waendelee kuzoa takataka kama kawaida ,kilichofanyika na nini la Arusha ni kutoa barua ya kusudio la kuingia milataba rasimi na wazoa taka katika maeneo mbalimbali"Alisema
Mtanda aliwaagiza maafisa tarafa kumpelekea majina ya mkandarasi walioacha kukusanya takataka ili awashughulikie kwasababu bado wana mkataba wa kuendelea kuzoa taka ngumu katika jiji la Arusha
Mkuu huyo wa wilaya ameahidi kumwandikia barua mkurugenzi wa jiji la Arusha, Hargeney Chitukulo, kumtaka zoezi hilo lisitishwe mara moja ili afanye thasimini ya kina kujua mkandarasi gani anastahili kupata kandarasi hiyo kwa kufuata kigezo cha utendaji bora wa kazi ikiwemo ukusanyaji wa fedha za serikali.
"Nitamtaka Mkurugenzi afanye tathimini ya kina kuwa ni wakandarasi gani wanaofaa wa kujua wakandarasi gani walilipa vizuri fedha za serikali na wakandarasi gani wanadaiwa "alisema
Alimtaka Mkurugenzi wa jiji la Arusha kutazama upya mchakato wa tenda huku akizingatia mawakala wenye sifa ikiwemo wenye magari ya kufanyia kazi na wanaolipa vizuri mapato ya serikali .
Akiongea na vyombo vya habari ,ofisini kwake Mtanda amewatoa wasiwasi wakandarasi hao na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa bidii kuhakikisha jiji la Arusha linakuwa safi.
Pia alisema zoezi la kutangaza tenda mpya limekuwa na malalamiko mengi kwa mawakala wa taka huku baadhi ya wanasiasa wakitajwa kuingilia zoezi hilo kwa kuweka watu wao wasio na sifa kwa maslahi yao binafisi ,jambo ambalo alisema hakikubaliki.
Katika hatua nyingine mkuu huyo amewaonya baadhi ya mawakala wa taka ngumu ambao waliacha kukusanya taka kwa kisingizio kwamba tenda mpya zimetangazwa hivyo wanawasiwasi iwapo wanaweza kupata tena tenda hiyo,ambapo alisema watachukuliwa hatua kali.
Baadhi ya wakandarasi wa kuzoa taka ngumu katika jijini la Arusha Abdalah Mgongo alipongeza kauli ya mkuu huyo wa wilaya na kusema kuwa ni kauli ya kizalendo yenye tija kwa jiji la Arusha yenye lengo la kuleta usawa kwa makandarasi.
Alisema kwa sasa jiji la Arusha linapaswa kuwa safi muda wote kutokana na watalii mbalimbali kumiminika baada ya rais Samia kutangaza utalii kupitia filamu ya Royal Tour hivyo linahitaji mawakala wazalendo wa kuzoa taka ngumu bila kujali maslahi yao.
Ends....
2 Comments
Mmh ... fight that will never get to End
ReplyDeleteExodûs 14;14
ReplyDelete