Na Joseph Ngilisho, ARUSHA
Kamati ya kuratibu zoezi la Sensa wilaya ya Arusha likiongozwa na mkuu wa wilaya Said Mtanda imewafukuza kwa aibu vijana 10 waliojihusisha na udanganyifu katika maombi yao ya kuhesabu sensa baada ya kubaini hawakuwa na sifa stahiki.
Akiongea na waandishi wa habari alisema kuwa kati ya waombaji 10,405 waliojitokeza,mahitaji yalikuwa ni watu 1777 na kati yao 10 waliondolewa na ameagiz uhakiki wa kina ufanyike ili kubaini udanganyifu uliojitokeza.
"Zoezi la kuhakiki bado linaendelea na hao waliochaguliwa hasijione wamepita huo sio msaafu bado tunahakiki na pale tunapojiridhidha kunaudanganyifu hatutasita kuwaondoa"alisema.
Alisema kuwa vijana walioondolewa alibaini baadhi yao walichomekwa bila kufuata utaratibu na wengine hawakuwa na vyeti walitumia vyeti vya ndugu zao .
"Mimi kwenye hili zoezi la Sensa sina ndugu yoyote niliyemchomeka, atakayejiridhisha kuwa mimi nimechangia kumwingiza mtu atoe taarifa nitamtoa mara moja staki udanganyifu kwenye zoezi hili na viongozi wote walionipigia niwaingize ndugu zao zikukubaliana nao maana staki kashfa ,wanisamehe sana"alisema Mtanda.
Aliongez kuwa mafunzo ya sensa kwa waliopita yataanz kesho kila siku mshiriki atalamba 50,000 kwa siku sita.
0 Comments