Na Joseph Ngilisho,ARUSHA
Chama cha walimu Mkoa wa Arusha(CWT)kimeitaka serikali kuhakikisha inaboresha maslahi bora ya walimu ikiwemo mazingira mazuri ya kufundishia na kulipa stahiki za walimu kwa wakati pindi wanapohamishwa vituo vya kazi.
Akiongea na waandishi wa habari katika kikao kazi cha wafanya maamuzi ngazi ya halmashauri na Mkoa,mwenyekiti wa CWT mkoani hapa,Mwl.Lotta Laizer alisema kuwa pamoja na Rais Samia Sululu Hasani kujitahidi kutatua baadhi ya changamoto ikiwemo nyongeza ya mshahara lakini bado hangamoto ni kubwa.
Laizer alisema kuwa serikali kama mwajiri wa walimu nchini inawajibu wa kuhakikisha walimu wanapata stahiki zao sahihi kwa wakati jambo litakalo saidia kuongeza morari wa kufundisha na kuongeza ufaulu nchini.
"Kuna changamota nyingi ambazo kimsingi mwalimu anastahili kuzipata ikiwemo,mfumo wa taarifa ,mabadiliko ya zama,kucheleweshwa kwa stahiki za walimu ,sheria kandamizi za kazi "alisema .
Hata hivyo alimpongeza Rais Samia kwa kuwaongezea mishahara walimu na kupunguza baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.
Katibu wa CWT,Abraham Kamwela,alisema kikao hicho kiliwashirikisha viongozi wa CWT Mkoa na wilaya ,wafanya maamuzi wakiwemo wakurugenzi wa halmashauri wakuu wa wilaya na makatibu wakuu wa wilaya ,maafisa elimu na utumishi lengo likiwa ni kufahamishana mabadiliko mbalimbali ya sheria.
"Kwa mfano sheria ya ajira na Mahusiano kazini inayo mabadiliko kadhaa inayohusiana na uendeshaji wa vyama vya wafanyakazi,hivyo tukikaa pamoja tunaweza kutafisiri mabadiliko hayo na kuondoka na Jambo moja"alisema.
Naye kaimu afisa elimu Mkoa wa Arusha,Shelley Swai alisema mkoa wa Arusha unachangamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa walimu wa shule za msingi na serikali.
Alisema mkoa wa Arusha unauhitaji wa walimu 8573 na waliopo ni 6738 tu,hivyo upungufu ni walimu 1793 .
Awali kaimu katibu tawala mkoa wa Arusha David Lyamongi alisema mkoa wa Arusha umekuwa ukifanya vizuri kwa matokeo mazuri ya ufaulu kutokana na jitihada zinazofanywa na wadau wa elimu
Lyamongi aliwasisitiza CWT kuweka mazingira mazuri na mahusiano baina ya serikali na chama Cha walimu ili kuondoa mivutano kati ya mwajiri na chama hicho hasa kuhusu suala la masilahi.
Ends...
0 Comments