ALIYEKATA RUFAA KUPINGA HUKUMU YA MIAKA 30,AFUNGWA JELA MAISHA


BY NGILISHO NEWS 

Mkazi wa Tandika jijini Dar es Salaam, Omary Lwambo, aliyekata rufaa kupinga kifungo cha miaka 30 jela badala yake ameongezewa adhabu kwa kufungwa maisha.

Mwaka 2017, Lwambo alitiwa hatiani na Mahakama ya Hakimu mkazi Temeke iliyomtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela kwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 12.

Mtoto huyo alikuwa ni mwanafunzi wa shule ya msingi wilayani Temeke na ushahidi uliotolewa mbele ya mahakama, ni kwamba mbakaji huyo alimfanyia mtoto huyo kitendo hicho zaidi ya mara 10, anapokwenda shule.

Ilielezwa kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo kati ya Januari na Julai 2016, huko eneo la Tandika Azimio, ambapo mfungwa huyo alikuwa akimsubiri mtoto huyo njiani akienda shule na kumpeleka nyumbani na kumlawiti.

Baada ya kumaliza haja zake, alikuwa anamsindikiza hadi shuleni na kumuombea kwa walimu kwa kuchelewa kufika, na mtoto aliweza kuelezea hadi maumbile ya mshtakiwa.

Walimu ndio waliogundua mtoto huyo kufanyiwa vitendo hivyo baada ya kumuona tabia yake imebadilika na hana furaha huku kiwango cha ufaulu alichokuwa nacho kikishuka ghafla.

ADVERTISEMENT


Mtoto huyo aliitwa na katika mahojiano, ndipo alipowaeleza kila kitu na kumtaja mshtakiwa huyo kuwa ndiye amekuwa akimfanyia kitendo hicho na pia akamtaja mwanafunzi mwenzake naye hufanyiwa.

Mshtakiwa alikamatwa na kushitakiwa ambapo Hakimu Mkazi Vicky Mwaikambo alimtia hatiani na kumhukumu kifungo cha miaka 30 jela, lakini akakata rufaa mahakama Kuu lakini Jaji Seif Kulita, aliitupa rufaa yake na kubariki kifungo hicho.

Kama ilivyokuwa katika adhabu ya kwanza ya kifungo cha miaka 30, mbakaji huyo hakuridhika na uamuzi wa Jaji Kulita na kuamua kukata rufaa mahakama ya juu zaidi na ya mwisho nchini.

Rufaa hiyo ilisikilizwa na majaji watatu -- Dk Gerald Ndika, Lugano Mwandambo na Pantrine Kente na kuitolea hukumu Julai 14, 2022.


Post a Comment

0 Comments