Na Joseph Ngilisho Arusha
Mwenge wa Uhuru jijini Arusha,Umezindua mradi wa kiwanda cha kuzalisha wadudu cha Chamzi ,watakaotumika kwa ajili ya virutubisho vya mifugo ,mradi ambao unathamani ya sh,milioni 550.
Msimamizi wa kiwanda hicho,Mayasa Mhina akiongea Mara baada ya mwenge kutembelea mradi huo,alisema ulianza Julai Mwaka 2021 kwa kuchakata taka na kisha kuzalisha protin ya mifugo.
"Tunapochakata taka tunazalisha wadudu ambao hutumika kama kirutubisho Cha Kuku,Samaki,Mbwa ,Nguruwe na Paka na pia tunazalisha mbolea asili ya shambani"alisema.
Aliongeza kuwa pamoja na virutubisho hivyo, ukusanyaji wa taka pamoja na kuchakata umeongeza kuzalosha ajira kwa wananchi katika jiji la Arusha .
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Sahili Geraruma alipongeza jitihada zinazofanywa na kiwanda hicho akidai ni ubunifu wa kiwango Cha juu ambao unasaidia kuhifadhi na kutunza mazingira na kuimarisha Afya za mifugo na mbolea kwa wakulima.
Katika hatua nyingine Geraruma ameridhishwa na mradi wa uzalishaji wa bidhaa mbalimbali kwa kutumia mazao ya nyuki wa kikundi cha vijana cha Sessan Enterprises huku akikitaka kikundi hicho kuwa mabalozi kwa wengine.
Akizundua mradi huo alisema katika halmashauri zote alizotembelea kikundi hicho kimekuwa na ubunifu wa kipekee kwani wengi wao bidhaa wanazozalisha zilikuwa zinafanana na kukosa utofauti.
Pia aliwataka vijana wengine kuiga mfano huo kwa kuunda vikundi kwa ajili ya kunufaika na mikopo ya halmashauri ya asilimia 10 na kuachana na tabia ya kulalamika kuwa ajira hakuna.
Kwa wale mliokwisha kunufaika na mikopo hii ya halmashauri hakikisheni mnarudisha kwa wakati kwani kuna faida ya kutekeleza hilo ni kupewa kimpaumbele pale wanapohitaji tena pamoja na kutengeneza mawasiliano mema.,"alisema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa mradi huo,Emmanuel Msafiri alisema wazo la mradi huo wa uzalishaji wa mafuta yatokanayo na asali ulianza mwaka 2019 na kutekelezwa na jumla ya vijana watano wakiwemo wakiume watatu na wawili wa kike ikiwa sasa unajumla ya vijana kumi.
Hata hivyo alisema mradi huo unatekelezwa na wanakikundi kupitia faida ya mauzo ya bidhaa zinazozalishwa na mikopo inyotokana asilimia 10 katika halimashauri ya jiji la Arusha kupitia mapato yake ya ndani.
Alisema mradi huo umechangia kiasi cha sh.milioni 6.595 ikiwa halmashauri ya jiji la Arusha imetoa takribani sh.milioni 30 kwa ajili ya kununua malighafi na zana mbalimbali za mashine za uchakataji wa bidhaa hivyo mradi umegahrimu takribani sh.milioni 36.595.
Ends....
0 Comments