Na Joseph Ngilisho Arusha.
Mtu mmoja aliyetambulika kwa majina ya Maulidi Suleimani (54)mkazi wa Muriet jijini Arusha amefariki dunia na mwingine kujeruhiwa mara baada ya kufukiwa na kifusi wakati wakipakia Moramu katika mlima Murieti ambao serikali ya wilaya iliufunga.
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,limetokea majira ya saa nne asubuhi wakati marehemu ambaye ni dereva wa lori lililokuwa likipakia Moramu na mwenzake wakiwa eneo la tukio.
Shuhuda huyo Amani Mbise alisema kuwa licha ya mgodi huo kufungwa na mkuu wa wilaya ya Arusha, Said Mtanda mapema mwaka huu baada ya kutokea kwa vifo vya namna hiyo ,bado baadhi ya wamiliki wa mgodi huo waliendelea kuruhusu shughuli za uchimbaji hatarishi.
Baba wa marehemu, Suleimani Maulid akithibitisha kifo cha mwanaye akidai kuwa alipigiwa simu na kuarifiwa juu ya tukio hilo na alipofika katika kituo cha afya cha Murieti ambako marehemu alikimbizwa kwa lengo ka kuokoa maisha yake ,alikuta tayari amehifadhiwa katika chumba cha maiti baada ya kupoteza maisha.
"Sijajua nini kimetokea lakini nimepigiwa simu na kuambiwa kuwa mtoto wangu amepata ajali na kupelekwa katika kituo cha afya cha Muriet ndipo nilipofika na kukuta amechaingizwa Mochwale ,amefariki"alisema.
Naye diwani wa kata ya Muriet, Francis Mbise akithibitisha kutokea kwa tukio hilo akidai kuwa alipigiwa simu na wananchi juu ya tukio hilo .
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Justine Masejo hakuweza kupatikana kuzungumzia tukio hilo.
Mwili wa mar3hemu umehifadhiwa katika chumba cha maiti katika kituo cha afya Murieti jijini Arusha ukisuburi uchunguzi wa tukio hilo.
Ends..
⁶
0 Comments