Ahukumiwa miaka 30 jela au faini Milioni 347

 Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha miaka 30 au faini ya Tsh. Millioni 347.872 Mkulima Mkazi wa Idodi, Bryton Kaundama (54) kwa kosa la kukutwa na pembe za ndovu zilizokuwa na thamani ya Tsh. Million 34. 7 ambazo alikuwa akiziuza huku akijua kuwa hiyo ni mali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mkuu Said Ally Mkasiwa amesema Mtuhumiwa alikamatwa Tareh 29/01/2021 ambapo Askari wa Hifadhi ya Ruaha walipata taarifa kutoka kwa Wasamari wema kwamba Mzee Kaundama anauza pembe hizo na wakaweka mtego wa kumkamata kwa kujifanya Kama Wateja wanaotaka kununua nyara hizo.

Baada ya Kukubaliana walikutana Eneo la Kidamali huku mzee Kaundama akiwa amebeba mfuko aina ya Shangazi kaja na pembe hizo zikiwa ndani yake na Kisha akakamatwa.

Mtuhumiwa aliomba kupunguziwa adhabu hiyo kwasababu ni kosa lake la kwanza lakini pia ana Familia kubwa ya Watoto 10 ambao wote wanamtegemea lakini hata hivyo Mahakama ikamuhumu kifungo cha miaka 30 au faini ya Shilingi Million 347.872.

Post a Comment

0 Comments